Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watoto Wanusurika Kula Sumu Iliyotegeshewa Mbwa

Kufuatia kitendo cha baadhi ya watoto kunusurika kula nyama yenye sumu iliyotegwa kwa lengo la kuua mbwa wanaozagaa katika mitaa ya mji wa Makambako, madiwani wa halmashauri ya mji huo wameibuka na kupaza sauti katika kikao cha baraza, wakitaka waangamizaji wa mbwa hao kutenga eneo maalumu la kutekelezea zoezi hilo sambamba na kuja na njia bora ya kuwanasa bila kuleta madhara kwenye jamii.

Wakihoji njia inayotumika kuua mbwa hao na hatari iliyopo kwa watoto wadogo mtaani, madiwani wa halmashauri ya mji wa Makambako, akiwemo John Ngimbuchi, diwani wa Kata ya Makambako, wanasema kitendo cha kutega nyama zenye sumu ili kuwanasa mbwa wazururaji kimekuwa hatari kwa maisha ya watoto kwani wapo waliokutwa wakitaka kuokota na kula nyama hizo. Hivyo, wanatoa agizo kwa watekelezaji wa zoezi hilo kuja na mpango mpya wa kuua mbwa hao.

Kufuatia malalamiko hayo, ndipo nililazimika kumtafuta kwa njia ya simu Bw. Samora Mgaya, Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji Makambako, ambaye anaeleza mafanikio ya zoezi hilo na kisha kukanusha madai ya viongozi hao kuhusu kutega minofu yenye sumu mitaani, akisema kuwa huwekwa kwenye maeneo ya mapori yenye mbwa wengi.

Mbali na tishio la mbwa wazururaji, baraza hilo pia limejadili changamoto ya shule yenye wanafunzi wawili tu na kuhoji kwanini isifungwe ili kupunguza gharama za uendeshaji, jambo ambalo limetolewa ufafanuzi na Afisa Udhibiti Ubora wa Shule wa Halmashauri ya Mji Makambako, Romanus Mlimila.

Wakati hayo yakijiri, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Juma Sweda, ametumia mkutano huo pia kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea mjini Makambako na kuathiri taswira yake.

Kuhusiana na mada hii: