Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Petroli Yapanda Bei Dar, Dizeli Yasalia

Watuamiaji wa vyombo vitumiavyo petroli watalazimika kuongeza Sh32 kwa kila lita katika bajeti yao ya kupata nishati hiyo kuanzia leo, huku watumiaji wa dizeli na mafuta ya taa wakiendelea kutumia bei zao zilezile.

Wanunuzi wa petroli kwa rejareja kwa mafuta yanayopita bandari ya Dar es Salaam wataongeza Sh32 katika kila lita ya mafuta watakayonunua Novemba mwaka huu lakini mafuta yanayopita katika bandari nyingine (Tanga na Mtwara) bei yake itasalia kama ilivyokuwa.

Taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliyotolewa inaonyesha kuwa sasa wakazi wa Dar es Salaam watanunua lita moja ya petroli kwa Sh2,752 kutoka Sh2,720 iliyokuwa ikitumika Oktoba mwaka huu.

Kwa watumiaji wa dizeli wataendelea kutumia Sh2,704 kwa lita moja ya mafuta kama ilivyokuwa Oktoba na mafuta ya taa wakiendelea kutumia Sh2,774 kwa lita.

Kwa wanunuaji wa rejareja kwa mafuta yanayopita Bandari ya Tanga sasa watanunua petroli lita moja kwa Sh2,813, dizeli Sh2,766 huku mafuta ya taa yakisalia Sh2,835.

Kwa Bandari ya Mtwara, petroli itaendelea kununuliwa kwa Sh2,844, dizeli kwa Sh2,797 na mafuta ya taa yakiendelea kusalia kwa Sh2,866 kama ilivyokuwa Oktoba mwaka huu.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: