Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Joyce Mwasumbi, mkazi wa Kijiji cha Kanazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge chumbani kwake.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kanazi, Rudis Ulaya amesema tukio la mwanamke huyo ambaye ni mke wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT, Ibrahimu Mwaipopo katika kijiji hicho kujinyonga limetokea Disemba 24, mwaka huu saa 2:00 asubuhi, baada ya mumewe kwenda kanisani kupalilia pembeni mwa jengo la kanisa hilo.
Chanzo; Itv