Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Kazi na Mahusiano kwa kushirikiana na Kampuni ya Kampuni ya Target Tours and Labour Surply Company Limited, imetangaza fursa za ajira kwa madereva wa pikipiki katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali leo Jumatatu Desemba 29, 2025, nafasi hizo ni kwa ajili ya vijana wa Kitanzania wenye sifa stahiki zikiwemo kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 37, pamoja na leseni ya udereva wa pikipiki katika madaraja ya A, A1 na A3.
Taarifa hiyo pia, inataja sifa zingine muhimu kwa waombaji wa fursa hiyo kuwa ni uzoefu usiopungua miaka miwili katika kazi ya uendeshaji pikipiki, mwenye elimu ya msingi au sekondari na awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiingereza.
“Mwombaji anapaswa kuwa mwanaume mwenye leseni ya udereva wa pikipiki na hati ya kusafiria,” imeeleza taarifa hiyo.
Ajira hizo ambazo zitakuwa chini ya Tasisi yaVelo Logistics Delivery services LLC huko UAE, zimeelezwa kuwa zitatolewa na kusimamiwa kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo na mshahara pia ukitolewa kwa sheria hizo.
Kwa wenye uhitaji wa ajira hizo, tangazo la Serikali limefafanua kuwa waombaji wanatakiwa kutuma wasifu wao (CV) kwa nia ya mtandao kupitia https://www.targettours.co.tz info@targettours.co.tz ikisisitizwa kuwa baada ya kutuma maombi hayo mwombaji atajisajili kupitia hpps://jobs.kazi.go.tz
Chanzo; Mwananchi