Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chalamila Afichua Utapeli Mpya Dar es Salaam

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataja baadhi ya wamiliki wa vituo vya kuuzia magari (showrooms) kuwa vinara wa utapeli, hususan dhidi ya wateja wa mikoani kwa kudanganya kuwa magari yao bado hayajatoka bandarini.

Uchunguzi umebaini kuwa wafanyabiashara hao huyatelekeza magari hayo katika maghala ya forodha (bonded warehouses) bila kuyalipia ushuru, jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa wanunuzi ambao tayari wameshalipia gharama za magari hayo.

Aidha, Bw. Chalamila ameonya kuhusu athari za mikopo chechefu inayojulikana kama "kausha damu," ambayo imekuwa ikisababisha wananchi kupoteza ardhi zao kwa dhuluma.

Amebainisha kuwa wananchi wengi huingia katika mikataba hiyo bila uelewa wa kutosha na kujikuta wakisaini makubaliano yanayowanyang’anya miliki za ardhi zao bila kujijua, hivyo amewataka kuwa makini na taasisi wanazokopa fedha.

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: