mbWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameviagiza vyombo vilivyopo chini ya wizara hiyo kufanya utafiti na kuja na suluhisho la kuondoa na kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi ikiwemo tuhuma za rushwa na kubambikiziwa kesi.
Pia amelitaka Jeshi la Polisi nchini kushirikisha makundi mbalimbali katika kutoa elimu ili kupambana na uhalifu.
Ametoa kauli hiyo katika ziara ya kikazi mkoani Kagera baada ya kupokea taarifa ya hali ya ulinzi na usalama ya mkoa huo iliyowasilishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, SACP Blasius Chatanda kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa kwa upande wake amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulinda amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu.
Chanzo; Global Publishers