Askofu Mkuu wa Kanisa la Biblia Tanzania, Daktari Stanslaus Komba amewataka wazazi na walezi kuzichunga familia zao na kutoiachia mitandao kulea watoto wao ili kujenga kizazi chenye maarifa ya kujituma, kuwajibika katika kazi na kumcha mungu kwa maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.
Askofu Komba ametoa wito huo, katika ibada maalumu iliyoambatana na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wanaolelewa na kanisa hilo kituo cha Mahenge Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Chanzo; Itv