Jaji mstaafu wa Tanzania Joseph Warioba amesema katika mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini humo kwamba kuhusisha vyombo vya usalama na siasa ni hatari.
Warioba ameihimiza serikali kukubali makosa yaliyotokea kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 ili kufungua njia ya maridhiano.
Amesisitiza pia juu ya umuhimu wa kujenga mifumo inayolinda uhuru wa vyombo vya usalama na kuhakikisha vinawajibika kwa mujibu wa sheria na wala sio kwa matakwa ya kisiasa.
Chanzo; Dw