Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Samia Atangaza Mapunziko Siku ya Uchaguzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitangaza siku ya Jumatano Oktoba 29, 2025 kuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika shughuli ya kupiga kura.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka imebainisha kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutangaza siku hiyo kuwa siku ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

“Kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi wenye sifa stahiki, wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi wa sekta binafsi, kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura, Rais amethibitisha Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya mapumziko,” imeeleza taarifa hiyo.

Hayo yanajiri wakati ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ikiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo.

 

 

Chanzo: East Africa Radio

Kuhusiana na mada hii: