Wanawake wawili Bi Ester Maua na Bi Dianola Jahi wakazi wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wamevuta hisia za wananchi wengi baada ya kila mmoja kujifungua watoto mapacha wanne, hali iliyofanya jumla ya watoto waliozaliwa kuwa wanane kwa akina mama hao wawili.
Kutokana na hali hiyo, jamii imeombwa kujitokeza kwa moyo wa upendo na mshikamano kuwasaidia akina mama hao ili kuhakikisha watoto hao wanapata malezi bora na huduma muhimu zinazohitajika katika hatua za mwanzo za maisha yao.
Chanzo; Eatv