Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tsavorite Madini ya Tanzania Yasiyojulikana

 Katika safu ya madini adimu ya vito yanayotambulika katika masoko ya Kimataifa, Tsavorite ya Tanzania imeendelea kujijengea nafasi ya kipekee, sio tu kwa uzuri wake wa kuvutia machoni, ubora wake, bali pia kwa hadhi yake ya kiuchumi na kimkakati.

Chini ya ardhi ya Kaskazini mwa Tanzania, hususan katika maeneo ya Milima ya Simanjiro iliyoko Kijiji cha Lemshuku, kunapatikana kito cha kijani ang’avu hadi kibichi kinachong’aa kwa mwanga wa asili, kikibeba urithi wa mamilioni ya miaka ya mabadiliko ya kijiolojia na fursa kubwa ya maendeleo ya taifa.

Katika ulimwengu wa vito vya kifahari (high-end jewellery), Tsavorite imejijengea sifa ya kuwa miongoni mwa madini ya vito yenye bei ya juu, hii ni kutokana na hali yake ya asili, ikiwa na rangi ya uang’avu wa kuvutia na inayoruhusu mwanga kupita kwa urahisi (transparency), ubora na ugumu (Mohs hardness) wake wa 7.0 hadi 7.5, Tsavorite ni imara zaidi kwa matumizi ya muda mrefu katika vito kama pete, hereni, mikufu, n.k, jambo linaloifanya kupendwa na wabunifu wa vito katika masoko ya Ulaya, Asia na Marekani.

Katika kutambua nafasi hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mikakati mahsusi ya kuhakikisha madini ya vito yanaongezewa thamani ndani ya nchi.

Mikakati hiyo inajumuisha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kukata na kung’arisha vito, kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wazawa kupitia Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kuboresha miundombinu na masoko ya vito, pamoja na kuweka Sera, Sheria na Kanuni zinazohimiza madini kuuzwa baada ya kuongezewa thamani hapa nchini.

Serikali kupitia Wizara ya Madini, Wachimbaji wadogo wa Tsavorite nao wamewekwa katika nafasi ya kipaumbele ambapo kupitia Programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT), Serikali imetoa leseni kwa zaidi ya wachimbaji wadogo (vijana na wanawake) 420 katika maeneo ya Mirerani na Lemshuku, kuwajengea uwezo wa uchimbaji salama na bora, na kuwawezesha kufikia masoko rasmi kupitia minada ya kitaifa na kimataifa inayofanyika kidigitali chini ya usimamizi wa Tume ya Madini kwa kushirikiana na Soko la Bidhaa – Tanzania Mercantile Exchange (TMX).

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: