Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mufti Asihi Wanaokashifu Uislamu Kupuuzwa

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally amewasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu nchini, Viongozi na Watanzania kuwapuuza wanaoeneza chuki za kidini mitandaoni, kuukashfu Uislam na kuibeza Quran ambapo amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuishi kwa upendo, umoja na kuvumiliana kama yalivyo mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W).

Mufti Zubeir amesema hayo wakati akitoa tamko la maazimio ya Kikao cha Baraza la Ulamaa kilichofanyika March 04, 2026 kwenye Makao Makuu ya BAKWATA ambapo amewasihi Waislamu kutokubali uchokozi kutoka kwa Watu wachache wanaochapisha ujumbe wa kumtukana Mtume, kuukashifu Uislamu na kuibeza Dini hiyo.

"Tunaamini kuwa wanaofanya hayo sio Wakristo wala sio Watu wa Dini nyingine yeyote bali Watu hao wana nia ovu ya kutuchonganisha ili tugombane na kutia mtafaruku kati yetu na dini nyingine na jamii kwa ujumla, nawasihi Waislamu wasiingie kujibizana kwasababu Watu hao wanataka kueneza chuki na fitna dhidi ya dini nyingine”

 

Chanzo; Millard Ayo

 

Kuhusiana na mada hii: