Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Vijana Zaidi ya 100,000 Watuma Maombi ya Tamasha la Vijana Urusi

Maombi toka vijana zaidi ya 100,000 yamepokelewa kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Kimataifa la Vijana (International World Youth Festival) linalotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu katika jiji la Yekaterinburg, nchini Urusi.

Kwa mujibu wa Grigory Gurov, Mkurugenzi wa Rosmolodezh, taasisi inayosimamia tamasha hilo, zaidi ya maombi 62,000 yametoka nchi 191 toka mabara ya Ulaya, Amerika Kaskazini, Kati na Kusini, Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na hata Australia.

“Lengo la Tamasha hili ni kupanua fursa za kujitambua kwa vijana, kuanzisha mahusiano ya kirafiki na kitaaluma, na kuanzisha miradi ya pamoja kati ya vijana wa Urusi na na wenzao wa mataifa mengine. Tamasha limepokelewa vyema duniani kote. Wataalamu tayari wameanza kuchambua maombi yaliyowasilishwa. Wanatarajiwa kuchagua washiriki 10,000 bora ambao watahudhuria tamasha hilo mnamo Septemba huko Yekaterinburg. Katika tathmini ya waliotuma maombi, kipaumbele kitatolewa kwa vijana wenye ujuzi, waliothibitisha uwezo wao na kutekeleza miradi yenye mafanikio katika mojawapo ya maeneo nane: sayansi na elimu, michezo, ujasiriamali, vyombo vya habari, teknolojia ya kidijitali na TEHAMA, tasnia za ubunifu, utawala wa umma na shughuli za kiraia. Aidha, motisha ya mshiriki katika kukuza ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana uzoefu pia itazingatiwa., alisema Grigory Gurov, mkuu wa Rosmolodezh.

Nchi zilizoongoza kwa kutuma maombi ni Morocco, Uzbekistan, India, Indonesia, Kyrgyzstan, Vietnam na Libya. Vijana watakaochaguliwa kushiriki kongamano hilo watagawanywa katika makundi ya sayansi, elimu, teknolojia ya kidijitali, ubunifu na tasnia za ubunifu, watengeneza maudhui, michezo na ujasiriamali.

Tamasha hilo lilianzishwa mwaka 2024 ikiwa ni baada ya Rais wa Urusi, Vladmir Putin kuagiza kuanzishwa kwa chombo kitakachowaunganisha vijana toka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kujadili mustakabali wao. Mmoja ya washiriki toka Tanzania alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Sentro, Ally Kashmiry.

Kuhusiana na mada hii: