Jeshi la polisi mkoani Kagera nimewashikilia watu 17 kwa tuhuma za uchochezi wenye viashiria vya kufanya vurugu mtandani
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda amedhibitisha kukamatwa kwa watu hao wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani humo na kusema kuwa wanaendelea na mahojiano na uchunguzi ukikamilia watapelekwa mahakamani
Pia Chatanda amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa upo imara siku zote na kusema kuwa wananchi wote ambao wamejiandikisha kupiga kura watapiga kura bila wasiwasi kwa sababu ulinzi umeimarishwa vizuri.
Chanzo: Clouds Media