Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mvua Zafunga Barabara Iyovi, Tahadhari Yatolewa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amefanya ziara ya kikazi katika eneo la Iyovi, wilayani Kilosa, kukagua hali ya usalama baada ya kifusi cha matope kuporomoka na kuziba barabara kuu ya Morogoro-Iringa. Changamoto hiyo imetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo, hali iliyosababisha kukwama kwa mawasiliano ya barabara na kuhatarisha usalama wa wasafiri na watumiaji wengine wa njia hiyo muhimu.

Akiwa katika eneo la tukio, Kamanda Mkama ametoa rai kwa madereva na wananchi wanaotumia barabara hiyo kuwa waangalifu na kuzingatia alama za usalama wakati huu wa dharura za kimaumbile. Amesisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari kubwa ili kuepusha ajali na madhara yanayoweza kujitokeza, huku juhudi za kuondoa kifusi hicho na kurejesha hali ya kawaida zikiendelea kwa ushirikiano wa mamlaka husika.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: