Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Serikali, Epukeni Safari Mashariki ya Kati

Serikali ya Tanzania imesema inaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali ya usalama inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati kufuatia mzozo kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na kwamba inawashauri Raia wa Tanzania wanaopanga kusafiri kwenda Mashariki ya Kati kuepuka kufanya safari hizo wakati huu na wale wanaoishi huko wabaki kwenye makazi yao wanamoishi.

Nchi hizo ni Bahrain, Israel, Kuwait, Qatar, Falme za Kiarabu (UAE) na Oman ambapo Serikali ya Tanzania imewahimiza Raia wote kuchukua tahadhari stahiki na kufuata maelekezo ya Mamlaka husika ambapo kwa Watanzania waliopo katika eneo la Mashariki ya Kati wanashauriwa kuepuka kufanya safari za kwenda au kutoka Mashariki ya Kati katika kipindi hiki, kubaki katika makazi mnayoishi inapowezekana na kufuata maagizo yanayotolewa na Mamlaka za maeneo husika na kuwa waangalifu wakati wote.

Ushauri mwingine ni kuepuka maeneo yenye shughuli za usalama/kijeshi katika maeneo mnayoish, kutumia njia rasmi za mawasiliano na taarifa, kuhifadhi pasipoti na vitambulisho vya Tanzania sehemu salama na inayopatikana haraka endapo kutatokea dharura “Serikali inawasihi Watanzania walioko Mashariki ya Kati kujisitiri kwa uangalifu na kuendelea kufuatilia mawasiliano rasmi ya Ubalozi na ya dharura”

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: