Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TRC Yaongeza Treni Kaskazini Kupunguza Mzongamano wa Krismasi

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza treni moja ya abiria kuelekea mikoa ya Kaskazini ili kupunguza msongamano wa wasafiri unaojitokeza kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na ongezeko kubwa la wasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya abiria kukosa usafiri au kulazimika kulala vituoni kutokana na uhaba wa vyombo vya usafiri.

Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TRC, Fredy Mwanjala amesema treni za MGR kwenda Arusha na Moshi ambazo kawaida husafiri kila Jumatatu na Ijumaa, sasa zimeongezewa safari ya ziada itakayokuwa ikiondoka kila Jumamosi kuanzia sasa hadi Januari 2026.

Amesema lengo la kuongeza treni hiyo ni kuhakikisha TRC inawahudumia ipasavyo Watanzania wanaosafiri kusherehekea sikukuu, wakiwemo watumishi wa umma na wanafunzi wanaokwenda na kurejea kutoka likizo za mwisho wa mwaka.

Kwa upande wa mikoa ya kati, Mwanjala amesema TRC itaongeza mabehewa kutoka 16 hadi 20 katika safari za Dar es Salaam–Kigoma baada ya kukarabati mabehewa manne, hatua inayolenga kukidhi ongezeko la abiria kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: