Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wakiwa kwenye foleni wakisubiri kupiga kura ya mapema katika kituo cha kupigia kura Sekondari ya Tumekuja Jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi.
Kwa mujibu wa Sheria Namba nne ya Uchaguzi yam waka 2018, imeelezwa kuwa kura ya mapema hufanyika kabla ya uchaguzi mkuu. Kura hiyo inawahusu watendaji wote wanaoshughulika na uchaguzi, walinzi na wasimamizi wa siku ya uchaguzi, ili waweze kutimiza majukumu yao bila changamoto zozote.
Chanzo; Mwananchi