Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Steve Nyerere Kuhusu Sakata la Niffer

Msanii wa filamu na Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere amewataka vijana kuwa waangalifu na nyakati ambazo serikali inapambana kuwaonganisha Watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu October 2025.

Amesema hayo yakiwa yamepita masaa machache Jeshi la Polisi litoe taarifa ya kumshikilia mfanyabiashara na Mwana Mitandao Niffer kwa madai ya kuhamasisha vurugu kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Steve ameandika “Angalia sana maisha yako. Utulivu ni njia ya mafanikio. Yawezekana kuna vitu huvipendi, lakini kuna utaratibu wa kuvipisha na kuviweka kando ili uwe na amani ya roho. Vijana wengi wameingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa kufuata mkumbo, wakiamini kuwa ‘mbona fulani anavuta, kwa nini mimi nisivute?’ Wakasahau kwamba madawa ya kulevya ni haramu na hayaruhusiwi.

Kufuata mkumbo kunaweza kukupoteza, ukajiona uko juu ya sheria. Kila ukiambiwa kuwa madawa ya kulevya ni haramu — kwa afya yako, kwa sheria za nchi, na hata kwa utamaduni wetu unapuuzia. Sikio halisikii likishajaa ujuaji.

Unakutana na wenzako, mnavuta, mnatoka nje mnavuta zaidi, mkisahau kuwa ni haramu. Ushujaa wa kweli si kutumia madawa ya kulevya, si kuharibu maisha yako kwa anasa.
Ushujaa wa kweli ni kusaidia familia yako, ni kupambana kutafuta riziki kwa bidii. Ukiweza kuitwa shujaa kwa sababu ya juhudi zako katika kazi na kujituma, kila mtu atakuheshimu.
Lakini ukijitafutia matatizo ukidhani utaitwa shujaa, mwisho wake unaiumiza familia yako na kujiletea maumivu.

Tuachane na madawa ya kulevya, vijana wa kike na wa kiume, na tuishi tukiamini hakuna aliye juu ya sheria.”

 

Chanzo: Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: