Taharuki yaibuka katika mtaa wa Viwandani kata ya Mjini Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga baada ya kichanga kukutwa katika mfuko wa taka na mfuga kuku, wakati akitafuta chakula cha kuku kwenye mifuko.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Oktoba 22, 2025 shuhuda wa kwanza wa tukio hilo, Jeremia Evance ameeleza kuwa huwa anapita kutafuta chakula cha kuku kwenye mifuko ya taka, wakati anafukua taka hizo ndio alipokutana na mtoto amewekwa kwenye mfuko,
“Huwa nina tenda ya kulisha kuku Nguzo nane, wakati na pitapita katika mifuko kutafuta chakula nikakuta mfuko ndani ya mfuko wa taka nilipoufungua nikakuta kichanga ndani, nilishtuka nikaenda kuwaita watu wanaokaa katika hosteli hii waje kushuhudia” amesema Evance.
Naye mkazi wa mtaa wa Viwandani, Stamili Mohammed ameeleza kuwa aliitwa kuja kushuhudia alipofika akakuta kweli ni kichanga kikiwa bado na damu mbichi, na aliyefanya tukio hilo amefanya leo si cha muda mrefu, kinaweza kuwa cha miezi saba au nane, maana viungo vyake tayari vimekamilika.
Chanzo: Mwananchi