Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watanzania Wataka Ulinzi kwa Wanawake Dhidi ya Ukatili

Ni matukio ya ukatili kwenye vyombo vya usafiri, barabarani na masokoni

Ripoti mpya ya utafiti iliyofanywa na Afrobarometer imebaini kuwa idadi kuwa ya Watanzania wanazitaka mamlaka husika hususan Jeshi la Polisi na Mahakama, kuongeza juhudi katika kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji katika maeneo ya umma.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo imebaini kuwa takribani asilimia 75 ya wananchi wanasema polisi na mahakama zinapaswa kulinda haki na usalama wa wanawake na wasichana, huku asilimia 60 wakisisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa kwa sasa hazitoshi na zinapaswa kuimarishwa kwa kiwango kikubwa zaidi.

Hata hivyo matokeo hayo ya utafiti yanahashiria kuwa, licha ya jitihada zilizopo, bado kuna hisia miongoni mwa wananchi kuwa mifumo ya ulinzi haijajibu kikamilifu changamoto zilizopo.

Kwa upande mwingine, utafiti unaonesha kuwa wananchi wengi wameripoti kuwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya umma ni machache au hayapo kabisa.

Takribani asilimia 11 ya Watanzania wanasema wanawake hukumbwa na unyanyasaji wa kijinsia “mara nyingi” au “kila mara” katika maeneo kama masoko, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri wa umma.

Hata hivyo, matukio hayo yanaripotiwa zaidi na wakazi wa mijini asilimia 15 ikilinganishwa na vijijini asilimia 9, pamoja na wananchi wanaokabiliwa na umaskini mkubwa.

Aidha, ripoti hiyo inaonesha dalili chanya za mabadiliko ya mitazamo ya kijamii, ambapo asilimia 70 ya wananchi wanasema wana imani kuwa wanawake na wasichana huaminiwa wanapotoa taarifa za unyanyasaji au ubaguzi.

Hata hivyo, wadau wanasisitiza kuwa imani hiyo inapaswa kuambatana na mifumo madhubuti ya kisheria na kiutendaji ili kuhakikisha haki inapatikana kwa vitendo.

Katika eneo la ajira, utafiti huo umebaini kuwepo kwa pengo kubwa la kijinsia. Wanaume wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na ajira ya kudumu kwa asilimia 44 ikilinganishwa na wanawake asilimia 28. Vilevile, takribani asilimia 24 ya wanawake walio katika umri wa kufanya kazi hawana ajira na wanaendelea kuitafuta, ikilinganishwa na asilimia 16 ya wanaume.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: