Watu wasiojulikana wamechoma Nyumba ya Polisi Kata wa Kata ya Chitete Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe na kuteketeza Mali ambazo zina thamani ya Shilingi Milioni Mbili wakati wa Polisi huyo yupo kwenye majukumu yake ya kikazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi Agustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema Nyumba hiyo ya Polisi Kata anayefahamika kwa jina la Nsajigwa Mwajeka ilichomwa mnamo 22 oktoba Mwaka huu.
Kamanda Senga amesema alipewa taarifa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Chitete Darkson Kamendu wakati Nyumba inaungua kwa sababu imeteketeza Vyumba viwili huku ndani kulikua na mali kama Nguo za kiraia , Vyombo vya nyumbani , Mahindi , Sare za Polisi, Kitanda, Godoro na Vitu vingine
Aidha Kamanda Senga amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika wamenaza Uchunguzi mara moja ili kuwabaini watu hao waliofanya kitendo pia amesititiza Tukio hilo lisihusishwe na mlengo wa Siasa.
Chanzo: Millard Ayo