Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thaddeus Ruwa’ichi, amesema hali ya afya ya Kardinali Policarp Pengo, sio nzuri kutokana na changamoto za kiafya zinazomkabili.
Taarifa ya Askofu Ruwa’ichi iliyotolewa leo, imetoa wito kwa Wakatoliki kumwombea Kardinali Pengo.
“ Mzee wetu mpendwa Kardinali Policarp Pengo anakabiliwa na changamoto za kiafya. Zimefanyika jitihada za kumsaidia kimatibabu hapa kwetu. Hata hivyo, imeonekana kwamba upo uhitaji wa kumpeleka nje ili apate matibabu ya uhakika zaidi.
“Kwa hiyo, mipango imefanyika ili akatibiwe India. Tunatarajia kwamba ataondoka siku za usoni kwa lengo la matibabu hayo. Ninawaalika nyote tuungane kumsindikiza kwa sala na matashi mema,” amesema Askofu Ruwa'ichi
Chanzo; Nipashe