Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Iran Mashakani Kushiriki Kombe la Dunia

Rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, amesema hajui kama Timu yao ya Taifa itaweza kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya nchi yake.

"Kilicho hakika ni baada ya mashambulio haya, hatuwezi kutarajiwa kushiriki Kombe la Dunia," amesema Taj akiiambia tovuti ya michezo Varzesh3 huku Iran ikishambuliana na Israeli kama sehemu ya vita vinavyoendelea.
Mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran yanaendelea baada ya kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, na hilo linaifanya nchi hiyo kutokuwa na uhakika na kuongeza hatari ya kutokuwa na utulivu wa ukanda huo wa Mashariki ya Kati.

Iran imepangwa katika Kundi G kwenye Kombe la Dunia na mechi zake itacheza jijini Los Angeles -- ambapo itakabiliana na New Zealand na Ubelgiji mnamo Juni 15 na Juni 21, kabla ya kucheza na Misri huko Seattle Juni 26, mwaka huu.

Marekani itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo pamoja na Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, mwaka huu.

Mashabiki kutoka Iran tayari walikuwa wamezuiwa kuingia Marekani katika awamu ya kwanza ya marufuku ya usafiri iliyotangazwa na utawala wa rais Donald Trump.

FIFA haikuwa tayari kutoa maelezo yoyote kutoka kwa Shirika la Habari la The Associated Press lililotaka kujua kuhusu hali ya sasa na ushiriki wa Iran katika Kombe la Dunia.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: