Klabu ya Yanga imemtambulisha, Pedro Goncalves kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho akichukua mikoba ya Roman Folz ambaye alitimuliwa.
Goncalves ametambulishwa usiku wa leo Oktoba 25, 2025 ikiwa saa chache baada ya Yanga kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ikiichapa Silver Strikers mabao 2-0.
Chanzo: Mwananchi