Marefa 17 wa Tanzania, wamepata beji za uamuzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwaka 2026.
Katika kundi hilo la marefa 17, idadi ya marefa wa kati ni sita, waamuzi tisa ni wasaidizi na wawili wa soka la ufukweni.
Kundi kubwa la marefa waliokuwa na beji za FIFA kwa mwaka huu 2025 wamefanikiwa kutetea beji zao kwa ajili ya 2026.
Ni mwamuzi mmoja tu ambaye ameshindwa kutetea beji yake naye ni Janet Balama na nafasi yake imechukuliwa na Dismas Respicious.
Marefa wa kati ambao watakuwa na beji za FIFA kwa 2026 ni Ahmed Arajiga, Nasir Siyah, Ramadhan Kayoko, Hery Sasii, Tatu Malogo na Amina Kyando.
Marefa wasaidizi ni Mohamed Mkono, Hamdan Said, Kassim Mpanga, Frank Komba, Ramadhan Ally, Dismas Respicious, Glory Tesha, Zawadi Yusuph na Mary Selemani.
Waamuzi wawili wa soka la Ufukweni ni Jackson Msilombo na Ally Mohamed.
Chanzo; Mwananchi