Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mo Salah, Marmoush Waibeba Misri Afcon

Timu ya taifa ya Misri 🇪🇬 imeanza mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa ushindi baada ya kuifunga Zimbabwe 🇿🇼 kwa mabao 2–1 katika mchezo uliochezwa jana.

Zimbabwe walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya mshambuliaji Prince Dube kufunga dakika ya 20, bao lililowapa matumaini makubwa mashabiki wao huku Misri ikionekana kusumbuliwa katika safu ya ulinzi.

Hata hivyo, Misri walirejea mchezoni kipindi cha pili ambapo Omar Marmoush alifunga bao la kusawazisha dakika ya 63, na kuamsha matumaini kwa mabingwa hao wa kihistoria wa AFCON.

Mchezo ulionekana kuelekea kumalizika kwa sare, lakini katika dakika za majeruhi, nahodha wa Misri Mohamed Salah aliibuka shujaa kwa kufunga bao la ushindi na kuipa Misri alama tatu muhimu katika mchezo wa kwanza wa kundi.

Kwa ushindi huo, Misri wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuwania kufuzu hatua inayofuata ya mashindano, huku Zimbabwe wakilazimika kupambana katika michezo ijayo.

Matokeo ya Mwisho:
🇪🇬 Misri 2–1 Zimbabwe 🇿🇼

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: