Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TFF Yatahadharishwa Kumfungia Kocha Katabazi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepinga kuendelea na usikilizaji wa kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Kocha Liston Katabazi kwa madai kuwa wanataka kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, iliyaoamuru kesi hiyo iendelee kusikilizwa.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, maarufu kama Mahakama ya Kisutu, na Hakimu Mfawidhi, Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, jana Jumatatu, Oktoba 21, 2025.

Kutokana na msimamo huo wa TFF mahakama hiyo imelazimika kusimama kuendelea na usikilizwaji wa kesi na badala yake imeiahirisha hadi Novemba 13, 2023.

Hakimu Kiswaga amewataka mawakili wa TFF, Makubi Kunju na Rahimu Shabani siku hiyo kuwasilisha mahakamani taarifa ya kusudio la kukata rufaa kama ushahidi wa kuthibitisha kwamba wako katika mchakato wa kukata rufaa.

Hata hivyo, Hakimu ametoa tahadhari kuwa kama mawakili hao hawatawasilisha mahakamani taarifa ya kusudio la kukata rufaa siku hiyo, basi mahakama itaendelea na usikilizwaji wa kesi.

Katabazi anayejitambulisha kuwa mdau wa soka na kocha wa mchezo huo mwenye leseni ya daraja C iliyotolewa na TFF alifungua kesi hiyo dhidi ya Wadhamini Waliosajiliwa wa TFF na TFF yenyewe mwaka 2024.

 

Chanzo: Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: