Lionel Messi alipokea zawadi ya nadra sana wakati wa ziara yake ya “GOAT Tour” nchini India saa ya kifahari ya RM 003-V2 GMT Tourbillon (Asia Edition) yenye thamani ya takribani TZS bilioni 2.6.
Saa hiyo ya kipekee, inayomilikiwa na watu 12 tu duniani, ilikabidhiwa kwa Messi na Anant Ambani, mwana wa bilionea wa India Mukesh Ambani, baada ya ziara ya Messi katika kituo cha uhifadhi wa wanyamapori cha Vantara.
Licha ya vurugu zilizotokea kwenye tukio lake la Kolkata, ziara ya Messi ilihitimishwa kwa kishindo na zawadi inayothibitisha hadhi yake kama GOAT wa soka
Chanzo; Global Publishers