Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kroos Amtetea Vinicius Jr Awashangaa Wanaomlalamikia

Kroos amepingana na wanaomkosoa Vinícius Jr, akisema hawajui hisia za kucheza mbele ya mashabiki 80,000. Kiungo huyo wa zamani wa Madrid amemtetea Mbrazil huyo, akisema hata yeye hakuwahi kufurahia kutolewa kwenye mechi.

“Ukicheza mechi kubwa kama hii, hasa ukiwa katika kiwango kizuri, ni kawaida kutofurahia kutolewa. Hata mimi sikuwa napenda kubadilishwa. Ingawa kwa uaminifu, sikuwahi kuondoka moja kwa moja kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.”

“Watu wanaweza kuhukumu kutoka nje, lakini napenda kusisitiza jambo hili, hakuna mtu anayeweza kuelewa hisia hizo isipokuwa yule aliye uwanjani, katika Clásico, mbele ya watu 80,000, timu ikiwa inaongoza 2-1, unataka kufanya kila kitu ila tu usitolewe. Hizo hisia ni ngumu kuelezeka, na wengi wanaokosoa hawajawahi kupitia hali kama hiyo.”

Katika mechi hiyo, Kylian Mbappé na Jude Bellingham walifunga mabao ya Real Madrid katika kipindi cha kwanza, huku Fermín López akipachika bao pekee la Barcelona. Mbappé alipata nafasi ya kufunga tena kipindi cha pili kupitia penalti, lakini shuti lake liliokolewa na Wojciech Szczęsny.

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: