Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Liverpool Kupoteza Bilioni 410 Wakishindwa Kushiriki UEFA

Klabu ya Liverpool inakabiliwa na uwezekano wa kupoteza hadi pauni milioni 120 (Bilioni 412) iwapo haitafuzu kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu ujao, kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya fedha za soka, Kieran Maguire.

kiasi hicho kinajumuisha mapato ya zawadi kutoka UEFA, haki za matangazo ya televisheni, mapato ya siku ya mechi pamoja na bonasi kutoka kwa wadhamini.

Kukosa kushiriki mashindano hayo ya kifahari barani Ulaya kunaweza pia kuathiri uwezo wa klabu kuvutia wachezaji wakubwa na kuingia mikataba mipya ya kibiashara yenye thamani kubwa.

Champions League imekuwa chanzo muhimu cha mapato kwa vilabu vikubwa Ulaya na kwa Liverpool kufuzu si tu suala la ushindani bali pia ni nguzo ya nguvu za kifedha kwa klabu hiyo.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: