Mshambuliaji wa Chelsea FC, João Pedro ameweka rekodi ya takwimu bora zaidi kwa mchezaji wa klabu hiyo tangu kipindi cha Diego Costa.
João Pedro amehusika moja kwa moja katika upatikanaji wa mabao 26 kwenye mashindano yote baada ya kufunga mabao 17 na kutoa asisti 9 akikaribia kuvunja rekodi iliyowekwa na Diego Costa.
Liam Rosenior
“Uwezo wa João unatisha, Ni mpiganaji ana akili ya ushindi, ubora na mabao."
"Ninampenda João,”
Uhamisho wa João Pedro umeonekana kuwa na athari kubwa kwa Chelsea na mashabiki wakianza kuamini anaweza kuwa mshambuliaji muhimu wa klabu hiyo katika miaka ijayo.
Chanzo; Bongo 5