Klabu ya Real Madrid imepanga kumuuza mshambuliaji wa Brazil, Vinícius Júnior, mwenye umri wa miaka 25, mwishoni mwa msimu ujao kufuatia mwenendo wake usioridhisha wakati alipotolewa uwanjani katika mechi ya El Clásico dhidi ya Barcelona.
Katika mechi dhidi ya Barcelona ambayo Real Madrid ilishinda kwa mabao 2-1 mwishoni mwa mwezi Oktoba, Vinicius 'alimuwakia' kocha wake, Xabi Alonso baada ya kumtoa wakati mechi ikiendelea, jambo lililowakasirisha viongozi na mashabiki wa timu hiyo walioanza kushinikiza auzwe kutokana na matukio ya kujirudia ya utovu wa nidhamu.
Vinicius Jr alijiunga na Real Madrid mwaka 2018 akitokea klabu ya Flamengo nchini Brazil, ambako alijulikana kwa kasi, mbwembwe na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira.
Chanzo; Global Publishers