Nahodha wa Nigeria William Troost-Ekong amesema Super Eagles wamepangwa katika kundi gumu kwenye fainali za mataifa huru ya Afrika ‘AFCON’ nchini Morocco lakini watakuwa makini sana kutokana na kumbukumbu mbaya za kukosa ubingwa katika AFCON ya mwisho iliyofanyika nchini Ivory Coast.
Super Eagles wamepangwa kundi C sambamba na Tanzania, Tunisia na Uganda huku beki huyo wa Al-Kholood ya Saudi Arabia amesema Nigeria ni miongoni mwa timu zinazowania ubingwa katika michuano hiyo hivyo wana kila sababu ya kupambana na kubeba taji hilo.
Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Disemba 2025 huku Ekong akiipa nafasi kubwa Nigeria kubeba taji hilo sambamba na Morocco ambaye ni mwenyeji wa michuano hiyo na mabingwa watetezi Ivory Coast
Chanzo: Eatv