Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher amekiri klabu yake hiyo ya zamani ipo kwenye kipindi kigumu baada ya kupoteza mechi nne mfululizo Ligi Kuu England na hivyo kuachwa pointi kibao na Arsenal iliyoko kileleni kwenye msimamo.
Mwanzo mzuri wa Liverpool kwenye Ligi Kuu England umekumbana na kisiki kwa siku za karibuni kutokana na kupoteza mfululizo na hivyo kuachwa nyuma kwa pointi saba na Arsenal.
Kikosi hicho cha Kocha Arne Slot kilianza kwa kupoteza mbele ya Crystal Palace na Chelsea kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.
Ligi iliporejea, ilijikuta ikipoteza mara nyingine mbili mfululizo dhidi ya Manchester United uwanjani Anfield na Brentford ugenini na hivyo kuifanya timu hiyo kuandika rekodi mbaya.
Liverpool imeonyesha udhaifu mkubwa wa kukabiliana na pasi za mipira mirefu, hasa ile inayopigwa kwenye boksi lao na wapinzani wametumia hilo kama fimbo ya kuwaadhibu.
Carragher amesema: “Kupoteza mechi nne mfululizo ni janga. Kuona mabingwa na tena waliofanya matumizi makubwa kwenye usajili wanakuwa kwenye hali hiyo, hilo ni tatizo.
Chanzo: Mwanaspoti