Gwiji wa zamani wa AC Milan, Ruud Gullit ametaja sababu ya kutomchagua nyota wa Barcelona, Lamine Yamal, katika upigaji kura wa tuzo ya Kopa (mchezaji bora chipukizi duniani), licha ya kinda huyo wa miaka 18 kuwa kipenzi cha wengi na mshindi wa tuzo hiyo mwaka huu.
Lamine Yamal alimshinda kinda wa Ufaransa na klabu ya PSG Desiré Doué wakati wa hafla ya tuzo ya Ballon d'Or, ziliyofanyika 22 Septemba 2025.
Gullit, ambaye alimkabidhi Yamal tuzo hiyo, amezungumza na kituo cha Ziggo Sport cha Uholanzi na kufichua kuwa alimchagua Desiré Doué badala ya Yamal, akieleza kuwa nyota huyo wa Barcelona tayari amefikia kiwango cha juu zaidi na hatakiwi tena kupewa msukumo.
Chanzo: Mwanaspoti