Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi (38) anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Inter Miami CF hadi mwaka 2026. Hatua hiyo inalenga kuendelea kuimarisha klabu hiyo inayomilikiwa na David Beckham, huku Messi akiendelea kuwa mhimili muhimu tangu alipojiunga mwaka 2023 na kuisaidia kushinda Leagues Cup.
Kabla ya Inter Miami, Messi aliwahi kuchezea Newell’s Old Boys nchini Argentina, FC Barcelona ambako alitumia zaidi ya miaka 20, na Paris Saint-Germain (PSG) kwa misimu miwili. Anabaki kuwa mchezaji bora duniani, akiwa na tuzo nane za Ballon d’Or na Kombe la Dunia alilotwaa na Argentina mwaka 2022.
Chanzo: Global Publishers