Mshambuliaji Marcus Rashford ameweka wazi kwamba anataka kuondoka kabisa Manchester United na kubaki Barcelona, baada ya msimu huu kumalizika.
Rashford alijiunga na Barcelona kwa mkopo kutoka Manchester United katika usajili wa majira ya kiangazi, na miamba hiyo ya Cataluña ina chaguo la kumsajili moja kwa moja msimu ujao.
Akiwa tayari amefunga mabao matano katika mechi 12, mashambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameweka wazi mustakabali wake kabla ya pambano kubwa la El Clásico dhidi ya Real Madrid litakalopigwa keshokutwa Jumapili, Oktoba 26.
Alipoulizwa na ESPN kama anataka kubaki Barcelona, Rashford amesema: “Ndiyo, bila shaka. Ninafurahia kuwa katika klabu hii na naamini kwa yeyote anayependa soka aneipenda klabu hii. Barcelona ni moja ya klabu muhimu katika historia ya mchezo huu. Kwa mchezaji, ni heshima kubwa kucheza hapa.”
Chanzo: Mwanaspoti