Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, amevunja ukimya na kueleza kiu yake ya kutaka kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026, lakini amesisitiza kuwa atausikiliza mwili wake kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 38, anayekipiga katika klabu ya Inter Miami ya Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), amekuwa akiibua maswali mengi kwa mashabiki wake ambao wanataka kumuona akicheza fainali hizo zitakazofanyika mwaka 2026 kwenye nchi za Marekani, Mexico na Canada.
Messi amesema kila mchezaji anatamani kucheza fainali za Kombe le Dunia kwa sababu ndio mashindano makubwa ya soka, lakini kwa upande wake hana budi kusubiri, na kuona kama mwili wake utamruhusu kuwa sehemu ya kikosi cha Argentina
Chanzo; Mwanaspoti