Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Kocha wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi, raia wa Argentina, kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Uteuzi huo umefanyika baada ya mkataba wa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco kusitishwa kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo, Novemba 4, 2025, mazungumzo rasmi kati ya TFF na uongozi wa Singida Black Stars yamekamilika.
Gamondi ataanza majukumu yake mara moja, akiiongoza Taifa Stars kuelekea kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba mwaka huu.
Chanzo; Global Publishers