Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha Mashabiki wa soka kutofika na silaha wala kutumia lugha za matusi katika mechi zitakazochezwa Oktoba 25 na 26, 2025 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Muliro Jumanne mbele ya Vyombo vya habari huku akigusia harakati za kampeni zinazoendelea “Tarehe 29 imekaribia ipo karibu sana na shughuli za Kampeni zinaendelea kwa wagombea mbalimbali waliopo katika level ya kitaifa, Wabunge na Madiwani Watu wote hawa wanalitegemea Jeshi la Polisi katika shughuli za kiusalama"
“Wakati shughuli za kampeni zikiendelea pamoja shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii, kesho na keshokutwa kutakuwa na mikusanyiko mikubwa Dar es salaam ambayo itafanyika uwanja wa Benjamin Mkapa".
“Tarehe 25 kutakuwa na mchezo wa soka wa Yanga dhidi ya Silver Strike kutoka Malawi, mchezo huu umekusanya hisia tofauti kutoka kwa Wapenzi wa soka kutokana na matokeo ya awali na unatarajia kukusanya Watu wengi kutokana na uongozi wa Yanga ulivyoamua uwe, uwanja unatarajia kukusanya Watu 60,000 na Watu hawa wakiwa ndani wanatakiwa waingie wakiwa salama na watoke wakiwa salama bila kujali matokeo yatakuwa ya namna gani"
Chanzo: Millard Ayo