Kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui, amesema kikosi chake na benchi la ufundi kwa ujumla walijiandaa kwa mwaka mmoja na nusu kwa ajili ya kucheza mechi ya ufunguzi katika michuano ya AFCON 2025.
Pazia la michuano ya AFCON 2025 limefunguliwa jana Jumapili Desemba 21, 2025 nchini Morocco ambapo kulikuwa na mechi moja kati ya wenyeji Morocco dhidi ya vijana kutoka visiwa vya Comoros iliyopigwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, jijini Rabat.
Mechi hiyo ya Kundi A ilimalizika kwa Morocco kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambayo yote yalipatikana katika kipindi cha pili dakika ya 55 kupitia kwa Brahim Diaz na dakika ya 74 lililofungwa na Ayoub El Kaabi.
Chanzo; mwanaspoti