Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Arteta Mambo Yazidi Kuwa Magumu, Mastaa Watatu Wagonjwa

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amethibitisha wachezaji wake watatu kupata majeraha kwenye mechi ya ushindi dhidi ya Crystal Palace kwenye Ligi Kuu England, jana Jumapili, Oktoba 26.

Eberechi Eze ndiye aliyefunga bao pekee katika mechi hiyo, alipowaadhibu waajiri wake wa zamani kuisaidia Arsenal kushindi 1-0 uwanjani Emirates.

Lakini, ushindi huo uligubikwa na majeraha ya wachezaji Declan Rice, William Saliba na Riccardo Calafiori, ambao wote walilazimika kutolewa uwanjani.

Wachezaji hao watatu wamekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Arsenal katika msimu huu, hivyo jambo hilo ni pigo kubwa kwa kocha Arteta. Arteta amesema: “William Saliba aliumia. Declan (Rice) naye aliumia pia.

 

Chanzo: Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: