Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanariadha JKT Washinda Medali Brazil

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesema linaendelea kuibua vipaji vya riadha kupitia timu yake teule iliyopo Kikosi cha Oljoro JKT mkoani Arusha baada ya wanariadha wake kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa nchini Brazil.



Praiveti Michael Sanga alishinda mbio za Sao Paulo International Marathon za kilomita 42 na kujinyakulia medali ya dhahabu kwa kutumia muda wa saa 2:14:17.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo alikuwa Praiveti Charles Sule aliyemaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2:44:45.



Msaidizi wa Kamanda wa Kikosi cha Oljoro JKT, Meja Masangara Maro, aliwapongeza wanariadha hao na kuwataka kuongeza juhudi na nidhamu katika mazoezi ili kuendelea kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Kwa upande wao, Sanga na Sule walisema mafanikio yao yametokana na nidhamu ya mazoezi na kujituma.



Kocha wa timu ya riadha ya JKT, Andrew Panga, aliwashukuru Watanzania kwa kuendelea kuhamasika kuunga mkono mchezo wa riadha na kusema Tanzania ina nafasi ya kupanda zaidi katika viwango vya riadha duniani.

 

Kuhusiana na mada hii: