Baada ya kukamilisha ziara ya wiki mbili Nchini China, takriban Wafanyabiashara 100, ambao ni Wateja wa Benki ya CRDB, wamewasili Nchini na kupokelewa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya.
Ziara hiyo iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Clouds Media Group kupitia programu ya Malikia wa Nguvu, imelenga kuwawezesha Wajasiriamali kupata maarifa, uzoefu na fursa mpya za kukuza biashara zao.
Akiwapokea, Dkt. Chaya amesema ziara hiyo imewapa Wafanyabiashara fursa ya kujifunza kuhusu uzalishaji, teknolojia, usimamizi wa biashara na namna ya kuunganisha biashara zao na masoko ya kimataifa, amesema Serikali iko tayari kuwasaidia watakaokuwa tayari kuwekeza katika maeneo maalumu yaliyotengwa.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Elizabeth Mgaya, amesema benki hiyo inaendelea kuwawezesha Wateja wake zaidi ya huduma za kifedha kwa kuwapa maarifa na fursa za kuongeza thamani katika biashara zao, amesema ziara hiyo inalenga kujenga Wajasiriamali imara, wenye ushindani na uwezo wa kutumia fursa za biashara ndani na nje ya Tanzania.
100 waliopelekwa China na CRDB warejea na Fursa
- Chanzo:
- Millard Ayo