Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Refa Atupwa Njee Ligi Kuu Kisa Yanga Vs Namungo

Mwamuzi Abdallah Mwinyimkuu ameshushwa daraja kufuatia maamuzi wa Kamati ya Waamuzi na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 kati ya Yanga na Namungo FC.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mwamuzi huyo kutoka Singida alishindwa kutoa uamuzi sahihi, ikiwemo kutafsiri sheria katika tukio la mchezaji Abdulkarim Kiswanya wa Namungo kuvutwa jezi na mchezaji Mussa Damaro wa Yanga ndani ya eneo la penalti.

Bodi ya Ligi (TPLB) imebaini kuwa Mwinyimkuu alishindwa kuchukua hatua stahiki kulingana na sheria, jambo ambalo ni mwendelezo wa makosa ya aina hiyo. Kabla ya hatua hii, mwamuzi huyo alikuwa tayari ameadhibiwa mwezi Desemba 2025 kwa kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitano.

Kanuni Iliyotumika: Adhabu ya kushushwa daraja imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: