Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TFF Yawachapa Rungu Mwalimu, Duchu

Mshambuliaji wa Simba Sc, Seleman MWALIMU 'Gomez' amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Tsh. Milioni moja kwa kosa la kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji Andy Lobulka Bikoko wa Dodoma Jiji wakati wa mchezo baina ya timu hizo uliopigwa katika dimba la Jamhuri, Dodoma.

Pia, Beki wa Simba David Kameta (Duchu) amepigwa faini ya milioni moja kwa kosa la kumwaga kimiminika uwanjani mara baada ya kufika katika uwanja wa New Amaan Complex kitendo kilichotafsiriwa kama imani za kishirikina.

Aidha Simba Sc imetozwa faini ya Tsh milioni tano kwa kosa la mashabiki wake kumrushia chupa za maji mchezaji William Edgar wa Dodoma Jiji wakati akitoka kiwanjani katika mchezo uliomalizika kwa sare tasa pamoja na kuwarushia chupa watoa huduma ya kwanza (Redcross) wakati wakitekeleza majukumu yao kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: