Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

FIFA Yamfungia Mchezaji kwa Kosa la Utapeli Bilioni 1

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemshusha rungu mchezaji wa kimataifa wa Algeria na klabu ya Espérance de Tunis, Youcef Belaïli, kwa kumfungia kutojihusisha na soka kwa muda wa mwaka mmoja.

📌 Nini kimetokea?
Belaïli amekutwa na hatia ya kutumia nyaraka za kughushi katika kesi ya madai ya kifedha dhidi ya klabu yake ya zamani, AC Ajaccio ya Ufaransa. Alikuwa akidai kiasi cha takriban Euro 380,000 (zaidi ya Sh1 Bilioni) kama bonasi.

💰 Adhabu alizopewa:
1️⃣ Kufungiwa mwaka mmoja (Kuanzia Machi 5, 2026).
2️⃣ Faini ya faranga za Uswisi 5,000 (Takriban Sh14.5 Milioni).

Hukumu hii ni pigo zito kwa staa huyo ambaye kwa sasa anauguza jeraha la goti, huku akipambana kurejea timu ya taifa ya Algeria kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026.

Mchezaji huyo ana nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

Kuhusiana na mada hii: