Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameongoza zoezi la kuiaga timu ya mpira wa kikapu ya Dar City hii leo Mei 20, 2026 inayoelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mashindano ya robo fainali za Mashindano ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL 2026).
Chalamila amesema kuwa endapo Dar City itafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali, yeye kwa kushirikiana na Viongozi wengine watatoa zawadi ya Shilingi milioni 50 kwa timu hiyo kama motisha.
Aidha itakumbukwa kuwa Dar City ilifanikiwa kufuzu hatua hiyo miezi kadhaa iliyopita nchini Afrika Kusini baada ya kushika nafasi ya nne katika msimamo wa kundi lao.