Njiani kutoka kwenye Tamasha la Kimataifa la Vijana (International Festival of Youth 2026) lililofanyika jijini Ekaterinburg, Urusi na kukutanisha washiriki toka mataifa 190, @ally_kashmiry amepiga stori na majirani Christine ambaye ni muandishi wa habari wa KBC na Tracy mwandishi habari wa The Star kuhusu kitu wamejifunza kwenye namna ya kupokea wageni namna nzuri ya kufanya branding ya matukio ili kufanya kila mwananchi awe balozi wa mapokezi na kuwafanya wageni wajisikie wako nyumbani.